Posts

Showing posts from March, 2022

SHIBE LiNAPUNGUA KILA KUCHAO

 Mbona niseme shibe linapungua kila kuchao?? Kwa nini nikaangazia tu shibe ,ni kwa sababu bila chakula binadamu Hana uhai Tena. Sasa hivi kilichokuwa Cha Bei ya chini ni Cha Bei ya juu iliyo maradufu ,Bei ambayo hairidhishi ,Wengi wanaulizana tufanye nini ,twende wapi ,tumlilie nani. Bei ya mafuta ya kupika haswa ndio kizungumkuti kwa sasa ,vitoe si vitoe Tena kwani havina ladha kwa sababu havipati mafuta ya kutosha, usafiri nao kwa upande wao umesema "wakipandisha tutapandisha" nauli unaenda kupanda kwa kiwango Cha ajabu sana ,Wengi watalazimika kutembea kwa mguu hata ikiwa safari ya Marekani. Athari ya kupanda kwa Bei ya bidhaa hapa nchini inamkosesha mwananchi usingizi ,hajui kesho atakula nini pamoja na wanae ,lawana zinawapata wazazi kwa kuwa tu watoto wao hawajapata Cha kuweka mdomoni ,itafikia wakti binadamu ataamua kumla binadamu mwenziye kwani yeye ndo chakula kilichobakia mbele na nyuma. Niulize tu ila kwa unyenyekevu ,uliyemchagua atetee maslahi yako Yuko wapi ?? U...

TUMWAMINI NANI?

  “TOA FUNGU LA ALFU KUMI UPATE KUOMBEWA “. HIZI NDIZO SEMI KUTOKA KWA VINYWA VYA BAADHI YA WACHUNGAJI WENGI HAPA NCHINI KWA WANAKONDOO WAO AMBAO WANATUMIKIA. ASHAKUM SI MATUSI ILA NIKISEMA HII NI NJIA MOJA YA WIZI AU NISEME VIPI. NINALOFAHAMU NI KWAMBA MAOMBI NI YA BURE KWANI MTU HUTOA SHUKRANI KWA MWENYEZI MUNGU KWA HIARI WALA SI KULAZIMISHWA ,KUMAANISHA MOYO UMEPENDA NA UKAKUBALI KUWA HIKI NILICHO NACHO MKONONI NAKITOA NIKIWA MWENYE FURAHA MBELE YA MADHABAO. NISEME NI KINAYA AU VINAYA KWANI MHUMINI ANISHI KWENYE NYUMBA YA MATOPE NA SI MATOPE TU KINGA YA JUU NI NYASI ZILIZOISHI MIAKA YAKE NA ZINAHITAJI KUTOLEWA ,MVUA IKINYESHA HANA MAHALA PA KUJIKINGA HIVYO INAMLAZIMU KIKIMBILIA KWA JIRANI ,NAE MCHUNGA KONDOO ANAISHI KWA NYUMBA ZA KIFALME.DAAH!! KONDOO ANAKUPA NGOZI ,NYAMA NA FAIDA ZINGINE LAKINI WEWE MCHUNGAJI HUNA HATA MUDA WA KUDHIBITISHA MAHALA AMBAPO KONDOO WAKO ANAISHI?. MTANIMALIZA JAMANI. ILISHANENWA TOKA ENZI ZILE YA KWAMBA WATAKUJA WENGI WASIO WA UKWELI KWA JINA...

AMANI IDUMISHWE

Image
  Siku zote binadamu tunafahamu umuhimu wa amani haswa hapa nchini Kenya .Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti tisa usisahau kuweka akilini kwamba sote tuna haki ya kuishi kama wakenya.Dhuluma za aina zote hazifai kuruhusiwa kwani hazina manufaa yoyote .Machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka alfu mbili na Saba yalileta picha zisizopendeza ,Wengi waliyapoteza maisha Yao bila kusudi lolote. Wafahamu amani ni nini??,umuhimu wa amani ni nini??.Basi amani ni kuhakikisha kwamba mwenzio au jirani yako yupo salama jinsi wewe upo salama ,mwazime mwenzio asiyenacho kwa sababu akikosa hakika hawezi akawa na amani moyoni mwake ,funza mwenzio kuhubiri amani popote aendapo .viongozi ni wa kuja na kuenda mimi na wewe ndio tutasalia pale tulipoachwa na kwa hivyo nifahamu mimi zaidi nami nikufahamu zaidi .Tuko kitu kimoja. Umuhimu wa amani siku zote ni kutakuwa manufaa katika nchi  Kwani shughuli ya kila mmoja ni kujenga nchi . Zaidi ya yote usisahau maombi ndio mwongozo mzuri wa kuhak...