AMANI IDUMISHWE
Siku zote binadamu tunafahamu umuhimu wa amani haswa hapa nchini Kenya .Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti tisa usisahau kuweka akilini kwamba sote tuna haki ya kuishi kama wakenya.Dhuluma za aina zote hazifai kuruhusiwa kwani hazina manufaa yoyote .Machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka alfu mbili na Saba yalileta picha zisizopendeza ,Wengi waliyapoteza maisha Yao bila kusudi lolote.
Wafahamu amani ni nini??,umuhimu wa amani ni nini??.Basi amani ni kuhakikisha kwamba mwenzio au jirani yako yupo salama jinsi wewe upo salama ,mwazime mwenzio asiyenacho kwa sababu akikosa hakika hawezi akawa na amani moyoni mwake ,funza mwenzio kuhubiri amani popote aendapo .viongozi ni wa kuja na kuenda mimi na wewe ndio tutasalia pale tulipoachwa na kwa hivyo nifahamu mimi zaidi nami nikufahamu zaidi .Tuko kitu kimoja.
Umuhimu wa amani siku zote ni kutakuwa manufaa katika nchi Kwani shughuli ya kila mmoja ni kujenga nchi .
Zaidi ya yote usisahau maombi ndio mwongozo mzuri wa kuhakikisha kuwa kila nchi ina amani. Mungu hawezi kupuuza kile alichokiahidi siku zote atakitimiza ,amekuwa nasi toka mwaka wa alfu mbili kumi na Saba na bado yupo nasi mpaka sasa hawezi akaruhusu nchi iangamie ana mipango mizuri kwa kila mmoja ,ikiwa yeye ni mpenda amani sembuse wewe usiyependa amani ,tusije tukakaidi kile ambacho tunajua ni cha umuhimu mkubwa kwani ni dharau hata kwa Muumba wetu.
Rangi zote za bendera ya kenya hazikuwekwa kama maridadi bali kutuongoza kwa njia inayofaa.
Unapoitazama bendera fahamu rangi nyeupe itatueleza mimi na wewe ni kitu kimoja ,rangi nyeusi inakukumbusha wewe bado ni mwafrika na unapaswa kujivunia kuwa mwafrika bila kusahau kujivunia uwepo wa mwafrika mwenzako ,nyekundu inakumbusha damu iliyomwagwa ila bado inakueleza damu hio haipaswi kumwagwa tena ,kijani kibichi bado inakukumbusha urembo wa nchi yako ya Kenya na hivyo lazima uitunze.
Jaribu kujenga twasira akilini mwako jinsi mandhari ya taifa letu yana uvutio wa kupendeza ,mbona tuiharibu nchi ambayo tumeijenga kwa miaka hamsini na zaidi kwa siku Moja ,haitawezekana tukishikana pamoja ,usiruhusu ndoto yako ambayo umetaka kuitimiza kwa miaka mimi ikatizwe ghafla ,litakuwa jambo la aibu sana.
Na usisahau kuwaombea ndugu zetu kutoka ughaibuni wanaopitia changamoto za ukosefu wa amani ni binadamu kama mimi na wewe Wana haki ya kuishi ,tuwe na Imani siku Moja kila kitu kitakuwa sawa.
Hakikisha unalifahamu hilo siku zote .Mungu yupo .
#AMANI IDUMISHWE

KAZI MURUA BRO
ReplyDeleteKazi nzuri bro
ReplyDeleteKazi njema
ReplyDeleteItadumu
ReplyDeleteπππ
ReplyDeleteKiswahili safii hongera kaka
ReplyDeleteHongera
ReplyDeleteAmaniπ―
ReplyDeletePeace
ReplyDeleteAmani tudumishe
ReplyDeletePeace all way
ReplyDeleteAmani!amani!Amani Kenya.Kazi nzuri sana kaka.Wakati ujao ufupishe kazi yako.
ReplyDeleteCool
ReplyDeletePeace and unity is all we want
ReplyDeleteπππ
ReplyDeleteGood one ka lasty
ReplyDelete