SHIBE LiNAPUNGUA KILA KUCHAO

 Mbona niseme shibe linapungua kila kuchao?? Kwa nini nikaangazia tu shibe ,ni kwa sababu bila chakula binadamu Hana uhai Tena. Sasa hivi kilichokuwa Cha Bei ya chini ni Cha Bei ya juu iliyo maradufu ,Bei ambayo hairidhishi ,Wengi wanaulizana tufanye nini ,twende wapi ,tumlilie nani. Bei ya mafuta ya kupika haswa ndio kizungumkuti kwa sasa ,vitoe si vitoe Tena kwani havina ladha kwa sababu havipati mafuta ya kutosha, usafiri nao kwa upande wao umesema "wakipandisha tutapandisha" nauli unaenda kupanda kwa kiwango Cha ajabu sana ,Wengi watalazimika kutembea kwa mguu hata ikiwa safari ya Marekani.

Athari ya kupanda kwa Bei ya bidhaa hapa nchini inamkosesha mwananchi usingizi ,hajui kesho atakula nini pamoja na wanae ,lawana zinawapata wazazi kwa kuwa tu watoto wao hawajapata Cha kuweka mdomoni ,itafikia wakti binadamu ataamua kumla binadamu mwenziye kwani yeye ndo chakula kilichobakia mbele na nyuma.

Niulize tu ila kwa unyenyekevu ,uliyemchagua atetee maslahi yako Yuko wapi ?? Una uhakika anapitia unayo yapitia  wewe?? anafahamu kweli kwamba Fulani aliniwezesha kuwa kiongozi?? Kweli tuko kwenye nchi yenye "TUMBOKRASIA". 

Shilingi na mwananchi kwa sasa ni kama binadamu na mafuta ,hawapatani kwa vyovyote vile ,mmoja yuwamtamani mwengine ila anayetamaniwa ila anayetamaniwa imekuwa vigumu kumpata kwa sababu vizuizi visivyo hesabika vimewekwa katikati Yao ,wakuviondoa vizuizi hivyo ndiye mstari wa mbele kuongeza vizuizi zaidi .

Siku ambayo tutafahamu maana ya utu basi hamna kitachoweza kuleta madhara kwa watu wetu ,mimi tushikane tusaidiane jinsi tutaweza kuiweka hii shilingi mfukoni na kuhakikisha vya dukani ili visije vikaoza lazima vishushwe Bei ili tuwe na uwezo wa kuvipata.

Sitasahau kukumbusha ,lazima tuombeane hata kama tuna dini tofauti ,yote yanawezekana.

Kutwegwa na gogo mara Moja haimanishi umekosea ,bali una nafasi nyingine.

       BARAKA!!!


Comments

  1. ...Naam,nakubaliana na hoja ambayo umeizungumzia jioni hii ,ila tunamuomba Mwenyezi atuajaalie tusije tukaangamia .Hata hivyo ,ni jambo la kusikitisha kuona vile viongozi ambao tuliwachagua sisi kutuwakilisha tayari wameshasahau kuwa huu ndio wakati wa kupigania masilahi ya wapiga kura kwao kwa njia mbali mbali kama kupanda bei kwa bidhaa na uchumi kudhoofika💔

    ReplyDelete
  2. Kazi kuntu kaka shibe lisipotee nataka kitambi

    ReplyDelete
  3. Wakenya watazidi kuumia tuna uongozi mbaya bei zinapanda wanasiasa nao wanapandisha joto LA siasa

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

TUMWAMINI NANI?