TUMWAMINI NANI?

 

“TOA FUNGU LA ALFU KUMI UPATE KUOMBEWA “. HIZI NDIZO SEMI KUTOKA KWA VINYWA VYA BAADHI YA WACHUNGAJI WENGI HAPA NCHINI KWA WANAKONDOO WAO AMBAO WANATUMIKIA.

ASHAKUM SI MATUSI ILA NIKISEMA HII NI NJIA MOJA YA WIZI AU NISEME VIPI. NINALOFAHAMU NI KWAMBA MAOMBI NI YA BURE KWANI MTU HUTOA SHUKRANI KWA MWENYEZI MUNGU KWA HIARI WALA SI KULAZIMISHWA ,KUMAANISHA MOYO UMEPENDA NA UKAKUBALI KUWA HIKI NILICHO NACHO MKONONI NAKITOA NIKIWA MWENYE FURAHA MBELE YA MADHABAO.

NISEME NI KINAYA AU VINAYA KWANI MHUMINI ANISHI KWENYE NYUMBA YA MATOPE NA SI MATOPE TU KINGA YA JUU NI NYASI ZILIZOISHI MIAKA YAKE NA ZINAHITAJI KUTOLEWA ,MVUA IKINYESHA HANA MAHALA PA KUJIKINGA HIVYO INAMLAZIMU KIKIMBILIA KWA JIRANI ,NAE MCHUNGA KONDOO ANAISHI KWA NYUMBA ZA KIFALME.DAAH!!

KONDOO ANAKUPA NGOZI ,NYAMA NA FAIDA ZINGINE LAKINI WEWE MCHUNGAJI HUNA HATA MUDA WA KUDHIBITISHA MAHALA AMBAPO KONDOO WAKO ANAISHI?. MTANIMALIZA JAMANI.

ILISHANENWA TOKA ENZI ZILE YA KWAMBA WATAKUJA WENGI WASIO WA UKWELI KWA JINA LA MUUMBA WETU .

WANATABIRI KISICHOWEZA NA HAKITAWAHI KUTIMIA KAMA BADO SISI MIMI NA WEWE TUNGALI TUNAISHI CHINI YA JUA ,WANAFANYA MIUJIZA AMBAYO HAIELEWEKI LAKINI SISI KINAKONDOO NI NANI TUNAKUBALI TU KWA KAULI MOJA BILA HATA KUJUA MADHARA YAKE.

NINACHOJUA MIMI NI IMANI YANGU INAYOWEZA KUNIPONYA SI MUOMBEZI ,HATA UKAOMBEWA MARA ALFU MOJA NA HAUNA IMANI HUWEZI UKAPONA LAKINI MENGI TUNAYOYASIKIA “MAMA/BABA LEO HII NAENDA KUKUPONYA UGONJWA WAKO USITIE SHAKA” BAADAYE WAULIZWA NI KILITOKEA “NILIOMBEWA NA MCHUNGAJI AKASEMA NITAPONA” ILHALI HATA MWENYEWE NDANI YA MOYO WAKO IMANI IKO CHINI ZAIDI.

SITAKI NILAUMIWE ATI NIMEMKUFURU MWENYEZI MUNGU ILA TENA KWENYE MAANDIKO NI MUNGU TU ,NAMWACHIA YOTE ,SIKU YA KIHAMA NI YEYE ATA AMUA.

KULA KILE AMBACHO HATA MBELE YA MACHO YA MUUMBA NI CHENYE HAKI NA TUENDELEE KUKUOMBA ATUSAMEHE KWA SABABU TUNAKOSEA KILA SIKU .

 

 

 

Comments

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Sina usemi ila nitakusoa ama nitakufumbua macho kuhusu fungu la kumi

    ReplyDelete
  3. ...Kwa uhakika waumini wengi wameachwa kwa njia panda kwenye imani yao ,Mungu atuhurumie lakini andiko takatifu pia limefafanua vyema jinsi ya kuzungumza na Mwenyezi moja kwa moja hivyo basi kila mtu anayo mamlaka ya kuamua njia atakayotumia kutatua shida zake,hata hivyo kazi nzuri mwanahabari ErickπŸ‘πŸ‘

    ReplyDelete
  4. Siku hizi kanisa imekuwa sehemu ya biashara wahubiri wametawaliwa na anasa ya pesa kila kitu hili wakufanyie maombo wanadai pesa huku wanadai kazi ya Mungu haiwezi enda bila pesa

    ReplyDelete

Post a Comment